Tuesday, August 9, 2016

Jose Mourinho ametumia nafasi ya utambulisho wa Paul Pogba kwa mara nyingine tena kuwapiga vijembe wapinzani wake kwenye ligi ya England.

Uhamisho wa Pogba umevunja rekodi ya usajili kwenye tasnia ya soka ulimwenguni.

Bosi wa Liverpool Jurgen Klopp wakati fulani aliwahi kunukuliwa akikosoa uhamisho huo, bila kusahau Arsene Wenger pia ambaye alinukuliwa akisema uhamisho kwa pesa nyingi kiasi hicho ni upuuzi.

Mourinho aliwajibu kwa kuwaambia kwamba, hawakuwa na maadili kutokana na kuzungumzia mambo yasiyowahusu.

Amesema: "Nafahamu vizuri mjadala unaoendelea, najua sana, wakati mwingine kwenye soka, mambo tofauti hutokea na vilabu huvunja huvunja rekodi, lakini haya yanawezekana kwa klabu kama Man United.

"Wakati niliposikia baadhi ya kauli kutoka kwa mameneja wakikosoa suala hilo, nikasema sidhani kama hawa watu wamewahi kuwa na tatizo kama hili kwasababu, ili kuwa moja kati ya vilabu vikubwa duniani, unahitaji kufanya hivi. Hivyo, kwa klabu kama Man United suala kama hili huweza kutokea."

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video