Kocha wa Manchester United Jose Mourinho ametetea uamuzi wake wa kumuondoa Bastian Schweinsteiger kwenye kikosi chake na kumpeleka kufanya mazoezi na kikosi cha vijana.
Mreno huyo amesema hayo kufuatiwa kuandamwa na watu mbalimbali akiwemo Mtendaji Mkuu wa Bayern Munich Karl-Heinz Rummenigge.
Mourinho amesema: "Kinachotokea sasa ndicho kinachotokea kwenye kila klabu ulimwenguni. Kwamba meneja anaamua kuchagua fulani ya wachezaji atakaowatumia kwenye msimu husika, na hili ndilo ninalolifanya.
"Ni kama ilivyoada tu tu kuwa na kikosi chenye wachezaji 20 jumlisha na makipa watatu, kitu ambacho nimekuwa nikikifanya kwa miaka 15 sasa. Lakini tuna wachezaji wengi sana, ushindani ni mkubwa sana hasa kwenye Ligi ya Europa.
"Unakuwa na risk nyingi kutokana na kusafiri mara kwa mara, kucheza mechi nyingi za Premier League. Hivyo nimefanya uamuzi wa kuwa na kikosi cha wachezaji 23 na makipa wawili, idadi ambayo ni kubwa. Mimi ndio mwenye maamuzi ya mwisho, ni rahisi tu kama hivyo."
0 comments:
Post a Comment