Zlatan Ibrahimovic amepewa mapumziko ya siku nne na kocha wake Jose Mourinho baada ya kucheza kila dakika ya mechi za kwanza za Manchester United msimu huu.
Msweden huyo ameshatupia kambani magoli manne katika mechi zake nne za kwanza, lakini Mourinho ameamua kumpa mapumziko kwa madai kuwa katika umri wa miaka 34 anatakiwa kupumzika.
"Huwezi kucheza mechi 70 kwa msimu. Kwahiyo nawapa mapumziko ya siku mbili baadhi ya watu ambao hawajachaguliwa kwenye timu zao za Taifa na nampa siku nne Zlatan". Mourinho amewaambia Mirror."Katika umri wa miaka 34 unatakiwa kupumzika".
"Nampa mapumziko. Inategemea na mazingira. Anacheza kila mechi na kila dakika".
"Kwa mechi nne amecheza dakika 360, nampa siku nne mtu huyo mkubwa".
Licha ya Mourinho kumuona kama umri umekwenda, lakini Zlatan haonekani kuwa mkongwe kila anapoongoza safu ya ushambuliaji ya United.
0 comments:
Post a Comment