Tuesday, August 30, 2016

Lionel Messi anaweza kuukosa mchezo wa kufuzu fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018 wakati timu yake ya taifa Argentina itakapovaana na Uruguay na Venezuela baada ya timu yake ya Barcelona kuthibitisha kusumbuliwa na maumivu ya misuli ya paja.

Taarifa kutoka ndani ya klabu ya Barcelona zinaeleza kwamba vipimo vya afya vilivyochukuliwa kutoka kwa nyota huyo vinaonesha  Messi ana matatizo ya misuli ya paja, lakini atasafiri kwenda kuungana na wenzake kwenye timu ya taifa huku akifanyiwa uchunguzi zaidi.

Ikumbukwe tu awali Messi alistaafu kuchezea timu ya taifa kabla ya kutangaza kuamua kurejea tena hivi karibuni.

Anatarajiwa kucheza dhidi ya Uruguay Jumamosi wiki hii na vilevile dhidi ya Venezuela Septemba 6

"Uwepo wake katika michezo yote hiyo utategemea na maendelea ya maumivu yake," taarifa kutoka ndani ya klabu ya Barcelona imeeleza.

Hili linaweza kuwa pigo kwa kiocha Edgardo Bauza baada ya kuwakosa nyota wengine Sergio Aguero na Javier Pastore.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video