Tuesday, August 2, 2016

Kwa takriban mwezi mmoja sasa, suala la uhamisho wa kiungo wa Juventus Paul Pogba limekuwa ni habari kubwa mno kutokana na pesa anayotajwa kutaka kununuliwa na Manchester United. Uhamisho wa Pogba endapo utafanikiwa kukamilika (suala ambalo ni kama tayari limekamilika bado kutangazwa tu), basi utakuwa uhamisho utakaovunja rekodi si tu kwenye klabu ya Manchester United, bali ulimwenguni kwa ujumla.
Mpaka mwisho wa wiki hii bila shaka Pogba (23) anatarajia kiuwa mchezaji wa United kwa mara nyingine tena, ikiwa imepita miaka minne tu tangu kuondoka kwake klabuni hapo teba bure baada ya mkataba wake kumalizika mwaka 2012. 
Wakiwa wamemshuhudia Pogba akiondoka kuelekea kwa miamba ya Italy Juve bila hata kupata moja ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza, United watakuwa wakijalaumu sana kutoa kiasi hicho cha fedha kumrudisha mwana mpotevu wao kwenye jiji hilo lililopo Kaskazini-magharibu mwa England.
Uhamoshi wake unakadiriwa kuigharimu United paundi mil 92. Kiasi hicho cha fedha kunamfanya Pogba ampiku Gareth Bale ambaye alinunuliwa kutoka Tottenham kwenda Real Madrd kwa paundi mil 86 mwaka 2013.
Dili hili la Pogba lilionekana kuchelewa, kwasababu kulikuwa bado kuna mkanganyiko kwamba ni klabu gani inapaswa kulipa pesa ya ziada kwaajili ya kumlipa wakala wa mchezaji huyo Mino Raiola. Sasa kwa minajili ya kumaliza haraka saga hilo, United wameamua kukubali kubeba mzigo huo wa paundi mil 20 kwajili ya kumlipa  wakala huyo wa Italy mwenye asili ya Kidachi na kufanya jumla ya fedha kuwa paundi mil 112.
Baada ya suala hilo kuwa limemalizwa, kinachofuata ni suala la maslahi ya mchezaji. Wakati kwa sasa Pogba anapata paundi mil 4 kwa mwaka kutoka kwa Juventus, sasa mshahara wake utaongezeka maradufu kwenye nyasi hizo za Old Trafford. Atakuwa akilipwa paundi 400,000 kabla ya kodi na baada ya makato atakuwa akipata paundi 220,000 na hivyo kumfanya kukusanya kitita cha paundi mil 20.8 kwa mwaka ukiachcna na madili mengine ya matangazo binafsi.
Kwa hiyo kwa mwaka Pogba atakuwa akivuta kitita cha jumla ya paundi mil 104, hivyo mpaka mkataba wake kumalizika atakuwa amejukusanyia kiasi cha paundi mil 216. Anakuwa moja ya wachezaji wanaolipwa kiasi kikubwa kwa wachezaji walionunuliwa miaka ya hivi karibuni kama Neymar na Bale.
Pogba aliondoka United kwa fedheha miaka minne iliyopita akiwa bwana mdogo mwenye kipaji cha hali juu. Lakini anarudi klabuni hapo akiwa ana makombe manne ya Serie A, anaingia kwenye listi ya wachezaji wanaolipwa pesa nyingi ulimwenguni na vile vile mchezaji aliyevunja rekodi ya usajili Manchester United na ulimwenguni kwa ujumla. 
Uhamisho huu wa Pogba unatoa funzo kubwa kwa wanasoka wengi hasa wa hapa nchini pengine na Afrika kwa ujumla kwamba, kufeli hatua ya kwanza si kufeli hatua nyingine. Muhimu ni kujituma na kutambua dhamira yako na malengo yako ili uweze kuyatimiza bila kujali changamoto unazopitia.
Pia ni fundisho kwa vilabu kuwa na subira kwa wachezaji wao ili kuweza kunufaika nao siku za usoni maana umri ni moja ya vigezo.
Pogba kwa sasa ana miaka 23, akiwa bado kijana mwenye safari ndefu. Aliondoka United akiwa na miaka 19 na sasa anarudi tena kama milionea.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video