Mlinda mlango mahiri Owen Chaima (pichani juu) ni mmoja wa nyota wa kikosi cha Mbeya City Fc kinachondoka leo hapa mjini Shinyanga kuelekea Mwanza tayari kwa mchezo mwingine wa ligi kuu ya soka Tanzania bara dhidi ya wenyeji Toto Africans uliopangwa kuchezwa jumapili hii kwenye uwanja wa CCM Kirumba.
Mapema leo asubuhi meneja wa kikosi hiki Godfray Katepa amesema maandalizi yote kuelekea mchezo wa jumapili tayari yamekalika kinachosubiriwa sasa ni dakika 90 za uwanjani siku hiyo ya mchezo ambazo anaamini zitakamilika kwa City kuibuka na ushindi na kubeba pointi tatu muhimu kabisa ambazo zitaisukuma timu yake kwenye nafasi nzuri katika msimamo wa ligi.
“Hakika tumekamilisha kila kitu kuhusu mchezo huo, hii ina maana kuwa maandalizi yote kwa vijana wetu yamekenda sawa, baada ya suluhu na Kagera Sugar tuliendelea kubakia Shinyanga lengo letu lilikuwa ni kupata wasaa mzuri wa kufanya mazoezi kwa utulivu, hilo lilifanikiwa tumefanya mazoezi ya kutosha kwenye uwanja wa Kambarage, kwa sababu tunakwenda mwanza leo tutakuwa na siku moja nyingine ya mazoezi ccm kirumba, hivyo basi hakuna shaka kuwa tuko kamili na tayari kwa mchezo wa jumapili”.
Kuhusu hali za wachezaji, Katepa aliweka wazi kuwa nyota wote wako kwenye hali nzuri kwa sababu hata baada ya mchezo na Kagera Sugar hakukuwa na majeraha yeyeto kikosini hivyo uhakika wa kucheza kwa kiwango cha juu na kushinda mchezo huo ni mkubwa kutokana na uimara wa wa chezaji hivi sasa.
“Timu yetu imeimarika zaidi, hatuna shaka na kupata ushindi dhidi ya Toto, vijana wako ‘fiti’ hakukuwa na majeruhi yeyote hata baada ya mchezo uliopita pamoja na mazoezi mazito ya siku kadhaa, tunasaifiri kwenda mwanza leo kwa lengo moja tu la kushinda ikiwezekana kwa idadi kubwa ya mabao”
0 comments:
Post a Comment