Monday, August 8, 2016

Ndugu Waandishi wa Habari, asalaam aleikhum.....Tumsifu Yesu Kristo..... Bwana Yesu asifiwe......Mwanakondoo ameshinda......

Naombeni kwa weledi sana, mihemko, mapenzi ebu kwa muda huu wekeni pembeni tujadili issues zenye mashiko kwa Watanzania, hususani soka!

Tushauriane, tuelekezane, tuelimishane ikibidi kwa reference za ndani na nje ya nchi Africa na Dunia.

Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu 2016/17 tayari ratiba yake imetoka, inaanza August 20.
Kikanuni, ratiba inaonesha mechi zitachezwa kwa mfumo wa nyumbani na ugenini. Nchi zote Duniani nadhani zinafanya hivyo katika ligi ya kwao.

Msimu uliopita, timu mbili zilikubaliana kuhamisha mchezo usichezwe uwanja wa nyumbani, ukachezwa ugenini lakini, ugenini ndio ukawa nyumbani. Hili lilipigiwa kelele sana, ikaonekana dosari kubwa mno katika ligi yetu! Hata juzi wakati mdhamini anakabidhi vifaa kwa timu zinazoshiriki ligi ya VPL msimu huu, lilikumbushwa kuonesha msisitizo kwamba, ni kosa kubwa ajabu ugenini kuwa nyumbani!

Ndugu zangu, hivi mna habari kwamba ipo michezo katika ligi yetu ugenini ni nyumbani na haizungumzwi wala kupigiwa kelele na yeyote? Au kwasababu ina wa fever hao wakubwa? Hivi ni haki kweli?

Kwa nini ugenini kuwe nyumbani kwa mtu?

Iliyopangwa ratiba ya nyumbani na ugenini nadhani kuna logic yake ndio sababu ile ya wale jamaa waliokubaliana msimu uliopita ugenini ikawa nyumbani ilipigiwa kelele wakimaanisha ukiwa nyumbani katika masuala ya mchezo kuna advantage zake!

Kwa nini kama kweli soka ni mchezo wa fair , kila timu isipewe haki yake ya michezo yake ya nyumbani ichezwe nyumbani? Kuipangia timu nyumbani halafu ikacheza ugenini kama nyumbani kwasababu yoyote ili ni kuipokonya haki yake ya kikanuni.

Timu kama Ruvu Shooting, JKT Ruvu, zenye kutumia uwanja wa Mabatini, Azam inayotumia uwanja wa Azam Complex , African Lyon inayotumia uwanja wa Karume, zinapocheza na timu za Yanga na Simba mechi zote huchezwa Taifa nyumbani kwa timu hizo kwasababu eti timu hizo zina washabiki wengi, viwanja vya nyumbani vya timu hizo havina uwezo wa kuwabeba!

Hivi kweli jamani! 
Juzi wakati Yanga anacheza na TP Mazembe, ilitoka amri ya idadi fulani tu ya wachezaji kuingia uwanjani na ilipotimia milango ilifungwa.

Kwa nini Klabu hizi zisitendewe haki hiyo kwa tiketi kuuzwa sawa na uwezo wa uwanja?

 Mabatini una uwezo wa kuchukua washabiki 7,000 ni wengi hao. Kwani wakati fulani tukicheza na timu hizo Taifa washabiki 7,000 hawafiki.

Ifike wakati, mazoea na faida binafsi tuweke pembeni tuangalie haki na matakwa ya kikatiba/kikanuni katika ligi yetu ili kuongeza ushindani na kuondoa manung'uniko na malalamiko miongoni mwa Klabu. Hili ni baya na lina lenga kuzibagua timu, nyingine zionekane bora, nyingine ovyo! Ni hatari sana hili. Nadhani muda wa marekebisho na mabadiliko katika hili ni sasa.

Nitafurahi sana, nikiungwa mkono katika hili. Lipigiwe kelele na Wadau wote tukiongozwa na wale waliolipigia kelele lile la makubaliano ya wawili wale msimu uliopita, ugenini ikawa nyumbani!

Nina mengi sana kuhusu suala hili, lakini niishie hapa nanyi ndugu zangu mlijadili kwa lengo la kujenga na kuleta usawa kwa timu zote katika ligi yetu.

President Malinzi namkubali sana, sana tu! Nitaeleza siku za usoni kwa nini namkubali Malinzi! Lakini Mtaaluma Boniphace Wambura pia ni miongoni mwa viongozi wa soka Tanzania ninaowaheshimu kwa usimamizi bora wa majukumu yao!
Ya Malinzi na Wambura, tutayajadili siku nyingine, ebu leo tujadili hii habari ya "Ugenini kuwa nyumbani"

Imetolewa na Masau Bwire
Afisa Habari Ruvu Shooting

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video