Thursday, August 4, 2016

Kocha wa Yanga Hans Van der Pluijm amesema kwamba hafurahishwi na mfululizo wa matokeo mabovu kwa timu yake kwenye Michuano ya Kombe la Shirikisho na kuahidi kufanya marekebisho kwenye mechi zijazo za kumalizia.
Pluijm ameogeza kwamba kutokana na hali hiyo anaamini kwamba mchezo wa kirafiki dhidi ya Mtibwa Sugar utamsaidia kwa kiasi kikubwa kujua mapungufu yao kabla ya kuwavaa MO Bejaia jijini Dar es Salaam.
"Katika mechi za ushindani, timu huitaji ushindi, mashabiki wetu wanahitaji kuona tukishinda, lakini hatuna matokeo mazuri katika Michuano ya Kombe la Shirikisho kwa kuwa kuna makosa ambayo tunafanya na yametugharimu. 
"Kama unavyoona hapa tunaendelea kujifua ili kuzuia makosa hayo yasijirudie kwa michezo ijayo." amesema Pluijm asubuhi ya leo mara baada ya program ya mazoezi kumalizika.
"Mchezo wa kirafiki dhidi ya Mtibwa sugar tunategemea utakuwa muhimu kwetu kama kipimo kujua wapi tuna kasoro kabla ya kuwakabili Mo Bejaia" alimalizia kocha mkuu Hans Van Pluijm.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video