Manchester United leo watakuwa nyumbani kwenye Uwanja wao wa Old Trafford kusaka ushindi wa pili mfululizo watakapokuwa na kibarua kizito mbele ya Watakatifu wa Saouthampton.
Katika mchezo huo utakapopigwa majira ya saa 4 za usiku, United wanatarajiwa kuingia na kikosi chao kamili akiwemo Paul Pogba ambaye mchezo uliopita hakuucheza kutokana na kutumikia adhabu ya kadi mbili za njano alizopata wakati akiwa Juventus ya Italy msimu uliopita.
Beki wa kati Chris Smalling pia atakuwepo kufuatia kuukosa mchezo uliopita kutokana na kutumikia adhabu yake ya kadi.
Kwa upande wa Southampton, nahodha wao Jose Fonte, ambaye amekuwa akihusishwa na mipnago ya kujiunga na United, anaweza kucheza licha ya kuukosa mchezo wa ufunguzi kufuatia kuchelewa kujiunga na wenzake kwenye 'pre-season'.
Ryan Bertrand atakosekana kutokana na kusumbuliwa na majeraha na nafasi yake itaendelea kuzibwa na Matt Targett.
Meneja wa Southampton Claude Puel, amezungumzia juu ya tetesi za mchezaji wake Jose Fonte kutakiwa na United: " Sina tatizo na Jose, il ni suala la ajabu kidogo kuona tetesi hizi zinakuja wakati tunakabiliana na mchezo dhidi ya United.
"Lakini mbali na hayo ni mchezaji mzuri na amecheza vizuri mazoezini... Jose ana uzoefu, hivyo hawezi kuchanganywa na masuala ya tetesi lakini kinachonishangazwa mimi ni kuona tetesi hizi zinakuja kabla ya mchezo wetu, siku mbili kabla ya mchezo."
Takwimu za mechi walizokutana
- Southampton wameibuka na ushindi wa bao 1-0 kwenye kila mchezo kati ya miwili iliyopita waliyocheza kwenye dimba la Old Trafford.
- Kabla ya hapo, ndani ya miaka 27 Southampton wamecheza michezo 19 ugenini dhidi ya United bila ya ushindi.
Manchester United
- United hawajafungwa nyumbani tangu walipopoteza dhidi ya Southampton January, ukiwa ni mfululizo wa mechi 11 kwenye ligi na michuano mingine ya ndani (wameshinda mara 8, droo tatu).
- Msimu uliopita United waliruhusu magoli tisa tu nyumbani, rekodi bora kabisa kuliko timu yoyote ya ligi kuu.
- Zlatan Ibrahimovic amefunga kwenye mchezo wake wa kwanza kwenye ligi nne za nchi tofauti-tofauti.
Southampton
- Waliruhusu magoli 19 kutikisa nyavu zao walipocheza ugenini, wakishika nafasi ya pili kwa rekodi nzuri nyuma ya Leicester walioruhusu magoli 18.
- Hata hivyo Southampton waliruhusu magoli kwenye michezo 13 mfululizo, ikiwa nimuda mrefu zaidi kucheza bila ya clean sheet tangu walivyofanya hivyo Novemba 2012 (mechi 21).
- Walifungana na West Ham kwenye kufunga magoli mengi ya vichwa kwenye msimu wa 2015-16 (magoli 15).
- Wafungaji wao bora wa msimu uliopita Graziano Pelle and Sadio Mane, wote wameondoka klabuni hapo- Pelle ameenda China, Mane ameenda Liverpool.
0 comments:
Post a Comment