Zlatan Ibrahimovic amecheza kwa mara ya kwanza kwenye dimba la Old Trafford akiwa kama mchezaji wa Manchester United walipocheza na Everton katika mchezo maalum kwa ajili ya Wayne Rooney ulioisha bila kufungana.
Mshambuliaji wa England Rooney (30), alicheza dakika 52 kabla ya kutolewa nje na mchezo kusimama kwaajili ya kupigiwa makofi na mashabiki takriban 58,597 waliohudhuria uwanjani hapo.
Zlatan, ambaye amejiunga na Man United mwezi July alitolewa dakika ya 65
Beki mwenye asili ya Ivory Coast Eric Bailly ambaye alinunuliwa kwa paundi mil 30 kutoka Villarreal, pia alicheza kwa mara ya kwanza katika dimba la OT.
"Usiku wa leo ni usiku ambao mimi na familia yangu tutaukumbuka sana," Rooney alisema baada ya mchezo kumalizika
Kocha wa zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson, ambaye alimsajili Rooney Agosti 31, 2004, na David Moyes ambaye alimfundisha Rooney kwenye klabu zote mbili walikuwepo
Zaidi ya hapo, kocha mpya wa England Sam Allardyse pia alikuwepo katika dimba la OT kumshuhudia Rooney, ambaye amefunga magoli 53 kwenye michezo 115 kwa taifa lake.
Rooney akiwekewa gwaride maalum kuanzia karibu na eneo la kuelekea kwenye vyumba vya kubadilishia nguo akiwa na wanawe watatu Kai mwenye miaka sita, Klay mwenye miaka 3 na Rooney mdogo mwenye umri wa miezi saba ambao walikuwa wamekaa mahali anapokaa Sir Alex Ferguson
Rooney, ambaye ni mchezaji wa zamani wa Everton amefungia United magoli 245 kwenye michezo 520 na kwa sasa anashikilia nafasi ya pili kwa rekodi ya ufungaji ndani ya klabu hiyo.
Rooney ameshinda makombe matano ya EPL katika kipindi chote alichodumu klabuni hapo, taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya, kombe moja la FA, na Fifa Club World Cup
Pia atakuwa akijaribu kuchukua Ngao ya Jamii kwa mara ya nne wakati timu yake itakapovaana na Leicester City kwenye dimba la Wembley Jumapili ijao.
Rooney ametangaza kwamba mapato yote yaliyotokana na mchezo huo yataenda moja kwa moja kwa watoto na vijana wasiojiweza nchini Uingereza.
0 comments:
Post a Comment