Manchester City imeendeleza wimbi lake la ushindi kwa asilimia 100% tangu kuanza kwa Ligi Kuu ya Englanda msimu huu baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya wabishi wa London West Ham United na kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo.
City walianza kupata mabao yao kupitia kwa Raheem Sterling mnamo dakika ya saba tu, kabla ya Fernandinho kuongeza la pili kwa kichwa dakika ya 18 baada ya mpira mzuri wa adhabu ndogo uliopigwa na Mbelgiji Kevin de Bruyne.
West Ham walipata goli lao la kufutia machozi kupitia kwa Michail Antonio dakika ya 58 baada ya kuunganisha krosi safi iliyochongwa na Arthur Masuaku.
Sterling aliongeza bao la tatu mnamo dakika 90 na kufanya ushindi wa mabao 3-1 kwa matajiri hao wa jiji la Manchester.
0 comments:
Post a Comment