Tuesday, August 9, 2016

SIMBA SPORTS CLUB
   DAR ES SALAAM.
         9-8-2016
TAARIFA KWA UMMA
Uongozi wa klabu ya Simba na benchi la ufundi,kwa pamoja unawashukuru sana wanachama,washabiki wake na watu wote waliokuja jana kwenye sherehe za miaka themanini ya klabu yetu,ambazo zilijumuisha kilele cha wiki ya Simba Day ambazo zilifanyika jana tarehe 8-8-2016 katika uwanja wa Taifa uliopo jijini Dar es salaam
Pia uongozi wa Simba unawashukuru sana kwa kwa ushangiliaji wenu wa 'NGUVU'uliochagiza ushindi mnono wa magoli manne kwa sifuri,dhidi ya timu kongwe kutoka Kenya AFC Leopards.
Washabiki wetu mmeonyesha tofauti kubwa baina yao na sisi,kuujaza uwanja kiasi kile kwa viingilio vyenu wenyewe,na sio kuingizwa 'BURE'ilhali timu imetoka ktk msimu ambao haukuwa na matokeo ya kuridhisha sana,ni ishara kuwa mna mapenzi makubwa sana na klabu yenu na uongozi unaamini hilo ni deni kubwa linalopaswa kulipwa kwa kuwapa furaha ktk msimu huu wa ligi 2016|17
Nitumie fursa hii pia kuwakumbusha wale wanaotubeza,eti Leopards inashika nafasi za chini kwenye ligi kuu ya Kenya.na ndio maana tukawafunga 4-0.wajiulize wao Medeama waliowapiga 'thalatha'walikuwa wanashika nafasi ya ngapi wakati wanawapa kile kisago cha mbwa mwizi?😀😃
Kimsingi timu mwalikwa kwenye tamasha la Simba Day lazma iwe inacheza ligi kuu ya kwao na iwe timu yenye historia ilioutukuka ktk soka..AFC Leopards ni timu iliopo ktk premier nchini Kenya na historia yake kwenye soka Afrika,huwezi kuilinganisha hata kidogo na Medeama ambayo iliwadhalilishaji 'WAKODISHWAJI'
Mwisho niwafahamishe kuwa timu yenu itaendelea na mazoezi kesho jumatano pale police kilwa road na weekend hii itaingia kambini,tayari kwa mchezo wa kwanza wa ligi kuu inayotarajiwa kuanza hivi karibuni.
Imetolewa na
HAJI S MANARA
MKUU WA HABARI
SIMBA SPORTS CLUB.
SIMBA NGUVU MOJA

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video