Magoli ya kipindi cha kwanza kutoka kwa Sam Vokes na Andre Gray yaliwapa ushindi wa nyumbani Burnely dhidi ya Liverpool baada ya kucheza mchezo mkubwa sana uliwashangaza majogoo hao wa jiji la Liverpool.
Nathaniel Clyne alifanya uzembe uliosababisha goli la kwanza baada ya Gray kuunasa mpira na kumpasia Vokes aliyeweka kambani mpira huo.
Steven Defour, ambaye alikuwa akicheza mchezo wake wa kwanza kwa Burnley alicheza kwa umahiri mkubwa na kutoa pasi ya goli la pili lililofungwa na Andre Gray.
Liverpool walimiliki mchezo kwa asilimia 81 na kupiga mashuti 26 ambayo hayakuzaa matunda yoyote golini kwa upande wa Vijogoo hao wa Anfield.
Kiwango cha umiliki mpira cha 19% kwa upande wa Burnley, ni kidogo zaidi kutokea kwenye Premier League tangu Opta ilipoanza kurekodi takwimu msimu wa 2003-04.
Ukiachana na mashuti mawili yaliyozaa magoli, Burnley walipiga shuti lingine moja tu ambalo hata hivyo lilitoka nje ya lango la Liverpool.
0 comments:
Post a Comment