Jurgen Klopp amepitia upya mipango yake ya usajili na sasa anajiandaa kurudi tena sokoni kutatua tatizo la safu ya ulinzi linaloikabili Liverpool.

Kocha huyo wa Majogoo wa Jiji wakati akiwa na timu yake mjini Los Angeles Marekani alionesha kwamba baada ya kusajili wachezaji saba, biashara yake ya usajili imekwisha, ingawa alishindwa kumpata mlinzi wa kushoto wa mabingwa wa EPL, Leicester City, Ben Chilwell.

Klopp kwasasa anajiandaa kumtumia James Milner kama beki wa dharura wa kushoto, lakini baada ya kuona beki wake wa kushoto chaguo la kwanza Alberto Moreno akiumia kwenye mechi waliyopoteza dhidi ya AS Roma , amethibitisha kuingia sokoni kama mchezaji anayemhitaji atakuwepo.
Liverpool ina majeruhi kama Mamadou Sakho, Joe Gomez na Joel Matip – ambao wote ni walinzi wa kati, wakati Lucas Leiva, ambaye anaweza kuziba nafasi hizo naye anaendelea kuimarika kutokea kwenye majeraha ya nyama za paja.

Kutafuta Mlinzi wa kushoto yalikuwa malengo ya Liverpool majira haya ya kiangazi na sasa bado wanaendelea kuhusishwa kumsajili beki wa Cologne, Jonas Hector kwa dau la paundi milioni 20.
0 comments:
Post a Comment