Nyota wawili wa miamba ya soka ya Hispania na mabingwa wa Ulaya, Real Madrid, Gareth Bale na Cristiano Ronaldo, na mmoja wa Atlético Madrid', Antoine Griezman, wamefanikiwa kuingia tatu bora ya kuwania Tuzo ya UEFA ya Mchezaji Bora wa Ulaya kwa Msimu wa 2015/16.
Shirikisho la soka Barani Ulaya UEFA limewatangaza watatu hao ambao watapigiwa Kura Alhamisi ya Agosti 25 huko Monaco wakati wa kuendesha Droo ya Kupanga Makundi ya UEFA CHAMPIONZ LIGI ili kumpata mmoja ambaye atatwaa Tuzo ya UEFA ya Mchezaji Bora wa Ulaya kwa Msimu wa 2015/16.
Washindi waliopita wa Tuzo hii ni Lionel Messi (2011, 2015), Andrés Iniesta (2012), Franck Ribéry (2013) na Ronaldo (2014).
Kama ilivyo kawaida ya Tuzo hii, Wanahabari kutoka Nchi 55 Wanachama wa UEFA ndio Wapigaji Kura ambapo kila mmoja huteua Wachezaji wake Watano Bora na yule ambae ana Pointi nyingi ndio ameingia kwenye Fainali ya hao Watatu wa mwisho.
Watatu walioingia Fainali:
Gareth Bale (Real Madrid & Wales)
Antoine Griezmann (Atlético Madrid & France)
Cristiano Ronaldo (Real Madrid & Portugal)
Nafasi nyingine:
4 Luis Suárez (Barcelona & Uruguay) – 29 points
5 Lionel Messi (Barcelona & Argentina) – 25
6 Gianluigi Buffon (Juventus & Italy) – 19
7 Pepe (Real Madrid & Portugal) – 9
8 Manuel Neuer (Bayern München & Germany) – 6
9 Toni Kroos (Real Madrid & Germany) – 5
10 Thomas Müller (Bayern München & Germany) – 2:
0 comments:
Post a Comment