Droo ya kupanga mechi za mtoano kuwania kufuzu hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa Ulaya imepangwa leo ambapo Manchester City watakabiliana na Steaua Bucharest ya Romania.
Safari hii Man City wanaanza safari ya Uefa Championz Ligi wakiwa chini ya kocha Pep Guardiola ambaye akiwa Mkufunzi wa Barcelona alishinda makombe mawili ya mashindano hayo makubwa Ulaya.
Man City wanajiandaa kutafuta nafasi ya kucheza hatua ya makundi kwa misimu sita mfululizo, lakini wanahitaji kujipanga kwani Steaua, ambao walimaliza nafasi ya pili kwenye ligi ya Romania msimu uliopita, waliwahi kushinda taji la kombe la Ulaya mwaka 1986 na wakashika nafasi ya pili mwaka 1989.
HAPA CHINI NI DROO NZIMA YA MECHI HIZO ZA MTOANO:
Ludogorets Razgrad (Bulgaria) v FC Viktoria Plzen (Czech Republic)
Celtic (Scotland) v Hapoel Beer-Sheva (Israel)
FC Copenhagen (Denmark) v Apoel Nicosia (Cyprus)
Dundalk (Republic of Ireland) v Legia Warsaw (Poland)
Dinamo Zagreb (Croatia) v FC Salzburg (Austria)
Steaua Bucharest (Romania) v Manchester City (England)
FC Porto (Portugal) v Roma (Italy)
Ajax (Netherlands) v Rostov (Russia)
Young Boys (Switzerland) v Borussia Monchengladbach (Germany)
Villarreal (Spain) v Monaco (France)
0 comments:
Post a Comment