Wekundu wa Msimbazi, Simba SC, jana walirejea jijini Dar es salaam wakitokea Chuo cha Biblia mjini Morogoro ambako waliweka kambi ya kujiandaa na ligi kuu Soka Tanzania Bara msimu wa 201672017.
Kikosi cha klabu hiyo kinachonolewa na kocha Mcameroon, Joseph Omog akisaidiwa na Jackson Mayanja, kimelazimika kuja Dar kwa lengo la kujianda na maadhimisho ya Siku ya Simba 'Simba Day' itayofanyika Agosti 8 uwanja wa Taifa na mwaka huu itakuwa maalum kwa Simba kutimiza miaka 80 tangu kuanzishwa kwake.
Simba kama ambavyo inafanya mara nyingi, imeweka kambi yake Hoteli ya Ndege Beach na Siku ya Simba Day itacheza na AFC Leopard ya Kenya iliyochokua nafasi ya Interclub ya Angola iliyojitoa kutokana na kubanwa na ratiba.
Ikiwa Morogoro ilicheza mechi nne za kirafiki, ilishinda 5-0 dhidi ya Burkina Faso, ikaichapa 2-0 Moro Kids, ikawabamiza 6-0 Polisi Morogoro na mchezo wa mwisho uliopigwa Jumatano ya wiki hii, Mnyama alikufa 1-0 mbele ya KMC.
Hata hivyo, vijana hao wa Msimbazi wanakuja wakati ambao Rais wa klabu hiyo, Evans Aveva yupo kwenye misukosuko dhidi ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ambayoJuzi ilimshikilia na kumlaza rumande katika kituo cha Polisi cha Urafiki kabla ya kuachiwa jana kwa dhamana.
TAKUKURU jana ilisema ilimshikilia AVEVA kwa kuwa fedha dola 300,000 zilihamishwa kutoka kwenye akaunti ya Simba katika benki moja, kwenda kwenye akaunti na benki nyingine.
Fedha hizo ni zile za malipo ya mwanasoka Emmanuel Okwi aliyeuzwa dola 319,212 lakini fedha hizo hazikulipwa mapema baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage kufanya haraka katika mauzo hali iliyofanya uongozi wa Simba ulioingia madarakani kuanza kuhaha kupambana na Etoile hadi kufikia Fifa ili walipwe.
0 comments:
Post a Comment