Friday, August 5, 2016


Wakati Azam FC ikiendelea kusisitiza Kipre Tchetche bado ni mchezaji wao, mshambuliaji huyo Raia wa Ivory Coast ameendelea kuwaweka njia panda mashabiki wa Wanalambalamba.
MPENJA SPORTS jana ilichapisha habari yenye picha ya Kipre akitambulishwa kwenye kikosi cha Al Nahdha ya Oman na kupewa jezi namba 10 kama ilivyokuwa Azam FC.
Baadaye Afisa Mtendaji mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba akatoa maelezo kwamba hawajui chochote zaidi ya kutambua Kipre bado ni mali yao na kama kuna klabu imemsajili, lazima itawasilisha nyaraka Chamazi.
Straika huyo ameibuka katika akaunti yake ya mtandao wa kijamii ya Instagram na kuwepa picha yake ikiambatana na ujumbe ambao unaonesha dhahiri ameiaga Azam FC.
Kipre katika ujumbe wake, amefurahia miaka mitano aliyoichezea Azam, huku akiwashukuru viongozi na mashabiki waliomuunga mkono katika kipindi alichofanya vizuri na asichofanya vizuri (Soma picha ya pili juu).
Nyota huyo aliyekuwa tishio kwa mabeki wa ligi kuu Tanzania Bara amebakiza mkataba wa mwaka mmoja na Azam FC na mpaka sasa hajaripoti mazoezini wakati wenzake akiwemo pacha wake, Michael Balou wakiendelea kujifua chini ya kocha Mhispania, Zeben Hernandez.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video