Bastian Schweinsteiger amesisitiza kwamba bado ana furaha kuishi jijini Manchester licha ya kutojumuishwa kwenye kikosi cha timu hiyo na kocha Jose Mourinho.
Mjerumani huyo ameondolewa na kuwekwa kwenye kikosi cha akiba na kocha Jose Mourinho, ambaye alithibitisha kwamba haihitaji tena huduma ya Schweinsteiger
Anatarajiwa kuondoka United mwishoni mwa dirisha hili la usajili na ametoa upadate nyingine kwa mashabiki wake
Kupitia ukurasa wake wa Twitter ametweet hivi: "Baada ya mizunguko yangu, nafurahia muda uliosalia katika siku ya leo hapa Manchester. Natumaini wote mna siku njema!"
United wanaonekana hawana mpango tena na Schweinsteiger na kaka yake Bastian, Tobi Schweinsteiger alinukuliwa akikosoa kitendo hicho alichofanyiwa mdogo wake na ku-tweet: "No respect."
Mpaka sasa, United wanaviungo wa kati watano ambao ni Paul Pogba, Michael Carrick, Morgan Schneiderlin, Marouane Fellaini na Ander Herrera.
Ripoti zinaeleza kwamba, klabu za AC na Inter Milan zinahitaji huduma ya Schweinsteiger, ambaye atatakiwa kupunguza sana mshahara wake endapo ataamua kuondoka.
Anatajwa kupokea kiasi cha paundi 200,000 kwa wiki.
Msimu uliopita, Schweinsteiger alianza kwenye michezo 21 na michezo 10 aliingia kutokea benchi.
0 comments:
Post a Comment