Saturday, August 6, 2016

Wanachama wa klabu ya Yanga leo wamemkodishia Mwenyekiti wa klabu hiyo Yusuf Manji kwa kipindi cha miaka 10.
Tukio hilo limetokea kwenye mkutano mkuu wa dharura uliofanyika kunako ukumbi wa Diamond Jubilee.
Katika kuonekana kuguswa na jambo hilo, Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo na mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe amendika maneno yanayoonekana kushangazwa na maamuzi hayo.
Zitto, ambaye ni shabiki mkubwa wa Simba ambapo hivi karibuni alitoa pia maoni yake juu ya namna Mohammed Dewji anavyotakiwa kuuziwa hisa, ameandika kwenye akaunti yake ya Facebook maneno haya: "WANACHAMA wa Yanga wamekubali kumkodisha klabu hiyo Mwenyekiti wao, Yusuf Manji kwa miaka 10 kuanzia leo.
Kandambili bana. Sijui akili zao wanaziazimaga? Sasa hizi ni akili au matope? Mnamkodishia mtu Timu? Kabisa? Kwa bei gani?"

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video