Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amefichua kwa kusema kwamba, Arsenal wamewasumbua msimu uliopita kutokana na kutumia mfumo wa moja kwa moja (direct style) na sio kutumia pasi nyingi.
Kwa miaka mingi Arsenal wamekuwa wakijulikana kwa soka lao la pasi nyingi na fupi fupi.
Lakini Klopp anaamini kwamba mwaka huu wa 2016 Arsenal watacheza aina ya soka ambalo wamekuwa wakicheza miaka nenda rudi.
“Nadhani kila aliyeangalia mchezo ule aliona utofauti kati ya mchezo huu na mingine ya nyuma," alisema huku akirejea mchezo ambao uliisha kwa matokeo ya sare ya 3-3 msimu wa 2015-16.
“Lakini kwa miaka michache iliyopita Arsenal wamekuwa wakicheza soka la moja kwa moja. Wana wachezaji wazuri lakini mwisho wa siku hawawatumii wote kila wakati wanapoanza kutengeneza mashambulizi, ni kitu cha kushangaza kidogo.
"Nadhani huo ni mpango wao wa kutaka kushinda mechi zao.”
Klopp anaaamini kwamba kudili na mipira mirefu ambayo inafika moja kwa moja kwa straika wao ni muhimu sana kwa timu yake kuliangalia kwa umakini.
“Arsenal mara zote imekuwa ni timu inayopenda kuchezea, mpira lakini mara ya mwisho tulivyocheza nao walikuwa wakipiga sana mipira mirefu na walikuwa wakimlenga Olivier Giroud," aliongeza.
“Mpira wa pili ulikuwa unamfikia Ozil, walisababisha matatizo mengi sana kwetu katika mchezo ule. Ilikuwa ni hatari sana.
“Tulijua hilo kwasababu timu nyingi sana zilichagua aina hiyo ya mfumo pale zilipokutana na sisi.
“Hakukuwa na hatari kutokana na walichokifanya ila hatari ilikuja kutokana na jinsi ambavyo waliutumia mfumo ule, kwasababu waliutumia kiwango cha juu sana hasa kwa namna Giroud na Mesut Ozil walivyocheza.”
0 comments:
Post a Comment