Saturday, August 6, 2016

Mesut Ozil, Laurent Koscielny na Olivier Giroud wote watakosa mchezo wa ufunguzu wa Lifi Kuu ya England dhidi ya Liverpool, kocha Arsene Wenger amethibitisha.

Watatu hao hawakushiriki mazoezi na wenzao baada ya Michuano ya Euro mwaka huu kumalizika na hivyo Wenger ameamua kutowajumuisha kwenye kikosi chake kitakachowaa vijana hao wa Jurgen Klopp kwenye dimba la Emitares.

Akiongea baada ya ushindi wa magoli 8-0 katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Viking jana, Wenger alisema: "Itakuwa mapema mno kuwachezesha katika mchezo dhidi ya Lverpool."

Kukosekana kwa Giroud kunamfanya Wenger kubakiwa na mastrika wawili ambao ni Theo Walcott na Chupa Akpom.

Walcott alianza kuziona nyavu kwenye mchezo wa jana dhidi ya Viking, huku Akpom naye akizidi kuonesha kile kinachotakiwa na straika kuelekea msimu mpya wa ligi baada ya kufunga goli lake la tatu katika michezo ya kirafiki.

Joel Campbell na Alex Iwobi walifunga magoli mawili kila mmoja. huku Santi Cazorla na goli lingine la kujifunga likiwazamisha Viking.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video