Wednesday, August 31, 2016

BAADA ya wachezaji saba wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, kujiunga na timu zao za Taifa, Kocha Mkuu Zeben Hernandez, ametumia mazoezi ya leo Jumatano asubuhi kuwasoma wachezaji wa timu kubwa waliobakia pamoja na wale wa timu ya vijana ‘Azam FC Academy’.

Zeben alitekeleza kazi hiyo kupitia mechi ya mazoezi baina ya timu hizo mbili, iliyomalizika kwa Azam FC kuwafunga wadogo zao mabao 3-0 yaliyowekwa kimiani ni kiungo Mudathir Yahya, mshambuliaji Shaban Idd na winga Ramadhan Singano.

Katika mchezo huo, wachezaji waliokuwa majeruhi Pascal Wawa na Aggrey Morris waliweza kucheza kwa vipindi tofauti, Wawa akiingia kipindi cha pili na Morris akianza mwanzo na kutoka dakika ya 60, wote wakionyesha kuwa wanakaribia kurejea dimbani kutokana na namna walivyocheza.

Akizungumza na mtandao rasmi wa klabu www.azamfc.co.tz mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo uliokuwa mkali na wa aina yake, Zeben alisema mechi hiyo ilikuwa na maana kubwa sana kwake, jambo la kwanza alitaka kuwaangalia wachezaji wake ambao hawajapata muda mwingi wa kucheza.

“Unajua toka tumealiza maandalizi ya msimu, kuna wachezaji wangu hawakupata muda mwingi wa kucheza na wengine hawajacheza kabisa katika mechi zinazoendelea, hivyo nilitaka kuwaangalia na kuwapa nafasi ya kucheza ili kuwaweka fiti,” alisema.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video