Hatimaye matamanio ya Eden Hazard kucheza nafasi ya mshambuliaji wa kati yameshapata mkunaji, Antonio Conte.
Kwa muda mrefu, Hazard amekuwa akicheza winga au nyuma ya mshambuliaji wa mwisho, lakini kocha mpya wa Chelsea, Conte, yuko tayari kumchezesha nafasi ya mshambuliaji wa mwisho.
Kuhusu Hazard kucheza mbele, Conte alisema: "Napenda kumuona akicheza nafasi hiyo, kama mshambuliaji. Linaweza kuwa suluhisho zuri kwetu. Anaweza kucheza kama winga-pia kama mshambuliaji wa pili".
Anatakiwa kujiboresha, lakini anafanya kazi kubwa ya kujiweka bora kama ilivyo kwa wachezaji wengine".
0 comments:
Post a Comment