Winga wa Chelsea Kenedy amekamilisha uhamisho wa mkopo kwenda klabu ya Watford.
Mbrazil huyo alijiunga na Chelsea msimu uliopita na kufanikiwa kucheza michezo michache.
Alifanikiwa kucheza michezo 20 msimu uliopita na kufanikiwa kufunga bao la mapema kabisa kwenye Ligi Kuu ya England akitumia sekunde 39 tu katika mchezo dhidi ya Norwich.
Hata hivyo, chini ya kocha mpya Antonio Conte, Kenedy amekuwa hana nafasi kabisa kwenye kikosi cha kwanza na hata sub.
Kuondoka kwa Kenedy kunaifanya Chelsea kuwa na jumla ya wachezaji 27 walio nje kwa mkopo, akiwemo Loic Remy ambaye mapema leo amejiunga na Crystal Palace.
0 comments:
Post a Comment