Friday, August 19, 2016

"Kikubwa ambacho nimekifuata hapo ni kuendeleza furaha yangu niliyonayo kwa miaka yote niliyoshiriki," amesema.

Usiku wa kuamkia leo, Usain Bolt ameshinda mbio za mita 200 kwenye Michuano ya Olimpiki Rio 2016 na kubeba medali ya dhahabu na kufanya awe na jumla ya medali nane za dhahabu tangu alipoanza kushiriki michuano hiyo.

Bolt amesema: "Sikuwa na furaha wakati nilipokuwa nimevuka mstari, lakini furaha yangu ilikuja baada ya kupata medali ya dhahabu- hicho ndicho kitu cha msingi sana."

Mpaka sasa ni Mmarekani Carl Lewis aliyekuwa akikimbia mbio fupi na Paavo Nurmi mbio ndefu ndio wanashikilia rekodi za kuwa na medali nyingi zaidi za dhahabu za olimpiki kwenye riadha.

Lewis alishinda medali za dhahabu tisa kati ya mwaka 1984 na 1996, wakati Nurmi pia alishinda tisa kati ya mwaka 1920 na 1928.

"Kitu gani kingine nifanye ili kuuthibitishia ulimwengu mimi ni bora? Najaribu kuwa moja kati ya wabora, kuwa miongoni mwa Ali na Pele," Bolt aliongeza.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video