Tangu kuwasili kwake kunako klabu hiyo, amekuwa akipata wafuasi wengi kutokana na aina ya soka lake la kuvutia analocheza.
Amekuwa msaada sana kwenye klabu ya Yanga hasa kwenye kuzuia, kushambulia pamoja na kutoa pasi za mwisho.
Kwa mujibu wa Kamusoko, leo amefikisha idadi ya followers 40,000 tangu afungue ukurasa wake wa Facebook.
Kuonesha kufurahishwa na jambo hilo, Kamusoko ameandika haya kwenye ukurasa wake huo wa Facebook: "40 000 followers now.... thank you all for your support you have been so marvelous ever since i opened this account.. May God bless you all enjoy your day."
0 comments:
Post a Comment