Sunday, August 28, 2016

Yanga leo ndio walikuwa wanafungua pazia la Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kukosa mchezo wa awali kufuatia kukabiliwa na michezo ya kimataifa.
Katika mchezo wa leo dhidi ya African Lyon wameweza kupata ushindi mnono wa mabao 3-0, mabao yaliyofungwa na Deus Kaseke, Simon Msuva na Juma Mahadhi.
Katika magoli hayo, moja ya waliotoa assist ni Thabani Kamusoko ambaye alitoa pasi ya goli la pili lililofungwa na Simon Msuva.
Kamusoko ni moja ya viungo hodari wa Yanga wenye mchango mkubwa sana hasa linapokuja suala la kusaidia kupeleka mashambulizi mbele, kusaidia kulinda, kutoa pasi za magoli na wakati mwingine kufunga kabisa.
Katika ukurasa wake wa Facebook Kamusoko ameandika hivi baada ya ushindi wa leo: "3 points 1 assist.... Good start⚽⚽."


0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video