Sunday, August 14, 2016

Yanga kwa mara ya kwanza jana walipata ushindi katika hatua hii ya makundi ya Michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuwafunga MO Bejaia ya Aljeria bao 1-0, bao pekee lililofungwa na Amissi Tambwe.
Ushindi huo umekata kiu kubwa ya washabiki na wachezaji kwa ujumla ambao walikuwa wakipambana kwa udi na uvumba kufanikisha jambo hilo.
Baada ya ushindi huo, kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Thaban Scara Kamusoko ambaye kwenye michuano hii amekuwa moja ya wachezaji wachache wa Yanga waliocheza kwa kiwango cha juu sana, ameandika ujumbe uliodhihirisha furaha yake kufuatia ushindi huo.
Kamusoko mwenye bidii sana ya kujifunza Kiswahili kupitia ukurasa wake wa Facebook ameandika hivi: "Thats what we needed most today.....to get ourselves confidence of going forward tusi kate tamaa....namuomba mungu kwa ushindi wa leo asanteni sana....ukifanya vibaya muombe mungu ata ukifanya vizuri muombe tena kwasababu ndo anajua kila kitu 👌👌⚽⚽💪💪."

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video