Mchezaji anayesubiriwa kwa hamu kutua Manchester United bado hajatua. Taarifa za vyombo mbalimbali vya habari zimekuwa zikitaja wachezaji ambao Jose Mourinho atawaondoa kwenye kikosi chake. Mapema Mata alitajwa sana lakini imeonekana sivyo.
Sasa kiungo wa timu hiyo Mjerumani Bastian Schweinsteiger ameonekana kuingia katika mkumbo huo.
Ripoti mbalimbali zinaeleza kwamba Schweinsteiger ameahamishiwa kikosi cha vijana cha timu hiyo kufanya nao mazoezi
Taarifa hizi hazijamfurahisha kaka yake Bastian hata kidogo
Amemwandikia ujumbe huu Jose
Tobi, ambaye ndiyo kaka wa Bastian ambaye alicheza kwenye ligi za madaraja ya chini nchini Ujeumani, ameonesha hisia kali juu ya kitendo alichofanyiwa mdogo wake. Kupitia mtandao wake wa Twitter ali-tweet hivi: ‘No respect (Si heshima).’ Tweet hiyo inamhusu moja kwa moja Mourinho baada ya kumfanyia ukaili huo kaka yake.
0 comments:
Post a Comment