Thursday, August 4, 2016

Jose Mourinho jana aliamua kukaa kwenye viti vya dharura badala ya vile maalum kwaajili ya benchi la ufundi katika mchezo maalum kwa Wayne Rooney kati ya Manchester United na Everton uliopigwa katika dimba la Old Trafford. 
Mourinho alikuwa na jopo lake lote kuanzia msaidiza wake Rui Faria na wengine kama Ricardo Formosinho na Silvino Louro.
Huo ndio ulikuwa mchezo wake wa kwanza kwenye dimba la Old Trafford akiwa kama kocha wa Man United na kushuhudia timu yake ikilizimishwa suluhu na Everton. 
Baada ya mchezo huo, Mourinho aliimbia MUTV kwamba ule ulikuwa ni usiku maalum kwa nahodha wake. 
'Ilikuwa ni maalum kwaajili ya Rooney, kwa mashabiki, sasa kwa mantiki hiyo, ilikuwa ni kwa nia ya kuonesha kuthamini mchango wake kama mchezaji ambaye amefanya makubwa klabuni hapa.
'Msimu ambao alijiunga na Man United ndiyo msimu ambao mimi nilikuja hapa England kwa mara ya kwanza, hivyo nilitamani sana kuwa naye, kila mtu anafahamu kuwa ni mchezaji ambaye nilimtaka mara nyingi tu. 
'Hatimaye sasa ninaye tena kwenye klabu ambayo anaipenda, timu ambayo ameichezea kwa mafanikio makubwa kwa miaka mingi.
'Lakini, nadhani bado kuna mengi mazuri yanakuja kutoka kwake kwasababu nahisi bado ana morali kubwa mno, furaha ya kupambana kila siku, ana furaha ya kuwa kiongozi wa wenzake uwanjani hasa vijana wadogo. Na ni mtu wangu pia, kwa sasa nina furaha kubwa kusema kwamba ni mtu wangu na natumaini kwamba atanisamehe pale nitakapombadilisha. 
'Ilikuwa ni lazima nimfanyie mabadiliko kwasbabu Jumapili tutakuwa na wachezaji ambao wanahitajika mchango wao kwa kiasi kikubwa.'

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video