Siku moja baada ya Waziri wa Michezo, Nape Nnauye kufanya mahojiano na Maulid Kitenge wa EFM akieleza kuunga mkono klabu za Tanzania kuwa Kampuni, C.E.O wa klabu ya Stand United Company LTD, Dr. Jonas Tiboroha amekiri kukunwa na kauli hiyo.
Nape alisisitiza klabu za Tanzania kubadilika, huku akiwaunga mkono wanachama wa Simba ambao wameridhia klabu yao kwenda kwenye mfumo wa kampuni ambapo wanachama watanunua hisa wakiongozwa na Mfanyabiashara maarufu na mwanachama pia wa klabu hiyo, Mohamed Dewji 'MO' ambaye anataka kununua asilimia 51 ya hisa kwa thamani ya Shilingi za Kitanzania, Bilioni 20.
Stand United nayo ilitangaza kwenda kwenye mfumo wa kampuni, lakini kumetokea mpasuko baada ya baadhi ya wanachama kugoma na kusababisha kuwepo kwa makundi mawili, Stand United wananchi na Stand United Kampuni.
Mgogoro huo bado unafukuta, hivyo Tiboroha aliyewahi kuwa katibu mkuu wa Young Africans amemuomba Waziri Nape kuangalia uwezekano wa kumaliza mgogoro huo.
Soma kauli ya Dr. Jonas Tiboroha hapo chini;
0 comments:
Post a Comment