Wednesday, August 17, 2016

Ni muda mfupi tu umepita tangu kocha mpya wa Manchester City kuanza kukitengeneza kikosi chake upya na kuingiza falsafa zake. Mara nyingi Guardiola anapoanza kutekeleza majukumu yake kwenye kila timu anayokwenda lazima kunatokea wahanga wa ujio wake.

Tayari tumeshaanza kuona kwenye klabu ya Manchester City Joe Hart na Yaya Toure wamenza kuwa wahanga wa ujio wa Guardiola.

Joe Hart, mlinda lango namba moja wa Timu ya Taifa ya England, nafasi yake imechukuliwa na Willy Caballero kuanzia kwenye mchezo wa ufunguzi wa ligi ya England dhidi ya Sundeland na ule wa jana wa mtoano kuelekea kufuzu kucheza makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Steaua Bucharest.

Toure, kwa upande wake, ameambiwa bado hajawa fiti kuingia kwenye kikosi cha kwanza cha kocha huyo, hivyo ahakikishe anakuwa fiti ili kuanza kupata nafasi.
Joe Hart alikuwa benchi kwenye mchezo dhidi ya Steaua Bucharest.

Hapa tunaangalia wachezaji mbalimbali ambao wamewahi kupitia misukosuko baada ya ujio wa Guardiola kwenye timu alizopita.

RONALDINHO
Legend huyu wa Brazil alikuwa moja ya wachezaji muhimu kwenye kikosi cha Barcelona kutokana na umahiri wake wa kufunga na kutoa pasi za magoli kwa kipindi cha miaka mitano alichokaa klabuni hapo.
Ronaldinho.

Lakini punde tu baada ya kukabidhiwa mikoba kwa Guardiola, Ronaldinho hakuwa tena na nafasi na kuamua kutimkia klabu ya AC Milan licha ya Manchester City kuonesha nia ya kumhitaji.

DECO
Deco alikuwa moja ya wachezaji muhimu kwenye nafasi ya kiungo kwenye misimu minne wakati wa kipindi cha kocha Frank Rijkaard. Uwezo wake mkubwa wa kupiga pasi uliifanya Barcelona kurudi kwenye hadhi yake ya kuwa klabu inayoogopwa Ulaya.

Lakini punde tu Guardiola aliposhika hatamu, alimuondoa kikosini na kuanza kuwapa nafasi baadhi ya wachezaji kutoka kwenye academy ya klabu hiyo. 

Alihamia Chelsea baada ya kusajiliwa kwa ada ya paundi mil 8 mwishoni mwa mwezi June 2008 - akiwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Luiz Felipe Scolari punde tu baada ya kuteuliwa kuwa kocha wa Chelsea.
Deco.

SAMUEL ETO'O
Samuel Eto'o alisajiliwa mwaka 2004 na kufunga magoli ya kutosha. Msimu mmoja kabla ya ujio wa Guardiola alianza kusumbuliwa na majeraha. Hata hivyo licha ya yote hayo, alifunga magoli 16 kwenye michezo 18 aliyocheza msimu huo.

Mwaka 2008 Guardiola aliamua kumuondoa Eto'o na nafasi yake kuchukuliwa na Zlatan Ibrahimovic, ambapo aina ya uhamisho wake ulikuwa ni wa kubadilisha (swap deal). Hata hivyo Zlatan naye hakuwa na wakati mzuri .
Samuel Eto'o.

GIANLUCA ZAMBROTTA
Beki huyo kisiki wa kulia mwenye asili ya Italy, alikuwa kwenye kiwango bora miaka miwili kabla ya ujio wa Guardiola akitokea kunako klabu ya Juventus. Lakini punde tu baada ya kuwasili kwa Guardiola, beki huyo hakuwa na nafasi tena na kuamua kurundi nchini Italy kukipiga kunako klabu ya AC Milan.
Gianluca Zambrotta.

YAYA TOURE
Toure amekumbwa na hali hii akiwa kwenye klabu ya Barcelona na sasa Man City. Akiwa Barcelona alicheza mismu miwili chini ya Guardiola, na kuisaidia timu hiyo kutwaa taji la La Liga na UEFA.

Lakini baadaye Guardiola hakuwa akimhitaji tena na kumwambia kuwa alikuwa huru kuondoka. Ilikuwa June 2010.

Aliamua kujiunga na Man City kwa ada ya paundi mil 24 na kuwa moja ya wachezaji tegemezi klabuni hapo kwa msimu yote na kuipa mataji ya ligi ya England pamoja, FA pamoja na mataji ya ligi.

Amekutana tena na Guardiola na kuanza kukutana na yaleyake aliyokutana nayo Barcelona
Yaya Toure enza zake akiwa Barcelona.


BASTIAN SCHWEINSTEIGER
Guardiola alitangazwa rasmi kuwa kocha Bayern Munich mwaka 2013 na ndani ya misimu yote miwili alimtumia Bastian Schweinsteiger kwenye kikosi chake cha kwanza klabuni hapo. Mara ya mwisho Bastian kuonekana Bayern ilikuwa ni Mei 23, 2015 wakati akicheza mchezo wake wa 500 kwa klabu hiyo.

Baada ya hapo Guardiola aliamua kuachana na kiungo huyo mkongwe ambaye aliitumikia timu hiyo kwa miaka 17 na kujiunga na Manchester United.
Bastian Schweinsteiger enzi zake akiwa Bayern Munich.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video