Joe Hart amerejea katika kambi ya timu ya Taifa ya Soka ya England akitokea Italia na leo atathibitishwa rasmi kuwa mchezaji wa Torino baada ya kila kitu kukamilika.
Joe Hart alipokelewa kwa kupewa jezi na skafu za Torino |
Golikipa huyo Jana alisafiri kwa ndege binafsi kutoka Manchester hadi Turin ambako alikwenda kuchukua vipimo vya afya na kufanya makubaliano ya kusaini mkataba wa mkopo wa muda mrefu na timu hiyo ya Seria A.
Nyaraka za mchezaji huyo kati ya klabu mbili, Man City na Torino zimekamilishwa Jana usiku na kabla ya dirisha la usajili kufungwa usiku wa leo, Hart atatangazwa kuwa mchezaji wa Torino.
Timu ya Torino itakuwa ikimlipa mshahara wa karibia pauni Elfu 55 kwa wiki, wakati Man City itamalizia kumlipa pauni laki moja na Elfu 30 zilizosalia kwenye mshahara wake.
0 comments:
Post a Comment