Golikipa wa Manchester City, Joe Hart, leo atapimwa Afya yake huko Italia ili ajiunge na Klabu ya Serie A Torino kwa Mkopo.
FA, Chama cha Soka England, kimemruhusu Hart kuondoka kwenye Kambi ya Timu ya Taifa ya England ili aende huko Italia
England hivi sasa ipo Kambini na Jumapili iko huko Slovakia kuchezea Mechi ya Kundi F la Kanda ya Ulaya kuwania kucheza Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Russia.
Hart, mwenye Miaka 29, alishaambiwa na Meneja wa Man City Pep Guardiola kuwa anaweza kuondoka.
Dili hii ya Hart na Torino inapaswa kukamilika kabla ya Jumatano Agosti 31 Saa 7 Usiku, Saa za Bongo, kwani hapo ndio Dirisha la Uhamisho linafungwa.
Guardiola hivi sasa huko City amekuwa akimtumia Kipa Willy Caballero na Juzi alimnunua Claudio Bravo kutoka Barcelona.
0 comments:
Post a Comment