Crystal Palace imeanza mazungumzo ya awali ya kumsajili Jack Wilishere kwa mkopo.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 22 amepata Ofa kadhaa kutoka klabu za ndani na nje ya England baada ya Arsenal kukubali aondoke kwa mkopo wa muda mfupi, lakini Palace wanapewa nafasi kubwa kufuatia jana mchana Wilshere kufanya mazungumzo na kocha wa timu hiyo, Alan Pardew .
Wilshere atafanya maamuzi yake ya mwisho leo wakat huu siku ya mwisho ya usajili ikielekea kumalizika.
Timu mbili za Italia, Roma na Juventus pia zimeonesha nia ya kumchukua mchezaji huyo wa England, Japokuwa nazo Bournemouth na Watford za ligi kuu ya soka ya England, zinaitaka saini yake.
Taarifa zinasema naye Pep Guardiola anaweza kumchukua Wilshere, lakini kocha wa Arsenal, Arsene Wenger hawezi kumpeleka timu kubwa kama Manchester City ambayo ni mpinzani wake wa moja kwa moja.
0 comments:
Post a Comment