MWINYI HAJI NGWALI HATUMII MADAWA YA KULEVYA, USHAHIDI HUU HAPA
Baada ya kuzagaa picha mbali mbali na taarifa kuwa mlinzi wa kushoto wa Yanga na Timu ya Taifa ya Tanzania Mwinyi Haji Ngwali “Bagawai” anatumia madawa ya kulevya taarifa hizo si kweli na wala hatumii Madawa yoyote mlinzi huyo.
Mwinyi Haji Ngwali hatumii dawa za kulevya na uthibitisho huo umetolewa na Awattif A. Abdulrasoul ambae yeye ni Mkemia Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Tarehe 09/05/2016 Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali ilipokea test tube moja ya damu na kikopo kimoja cha mkojo wa Mwinyi Haji kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa kitaalamu.
Uchunguzi ulifanyika kwa kutumia (Diffusion Assay Method na mult-line screen device test) umethibitisha kutokuwepo kwa ulevi ndani ya damu na aina yoyote ya madawa ya kulevya ndani ya mkojo.
Nae Haji Ngwali ambae ni baba mzazi na wakala wa Mwinyi amethibitisha kuwa mtoto wake hatumii madawa hayo na uthibitisho wa hilo alimpeleka kwa Mkemia mkuu wa Zanzibar na amethibitisha kuwa Mwinyi hatumii madawa hayo.
“Mimi na baba mzazi na wakala wa Mwinyi, huyu kijana hatumii aina yoyote ya madawa ya kulevya, nataka watanzania wajuwe kuwa kijana huyu hatumii tofauti na mitandao ya kijamii inavyosambaza taarifa za uzushi, mimi nipo tayari kwa mtu yoyote twende pamoja hospitali na kijana huyu tukampime kwasababu kama mtu anatumia madawa haya ataonekana tu hata kama kaacha kwa muda mrefu”. Alifunguka baba huyo.
Kwa upande wake Mwinyi amesema anaendelea vizuri afya yake tangu alipoumia katika mchezo dhidi ya Mo Bejaia ya Algeria ambapo kwasasa yupo fiti na anafanya mazoezi na wenzake.
“Nashkuru Mungu naendelea vizuri tangu nilipoumia kule Algeria na tayari nishaanza kufanya mazoezi na wenzangu na nipo fiti”.
Wakati huo huo Mwinyi amethibitisha kuwa kweli walikwenda kupima kwa mkemia mkuu yeye na babaake na ameonekanwa yupo salama.
“Ni kweli nilikwenda kwa Mkemia mkuu kupima mimi na babaangu na nimeonekanwa nipo salama, babaangu alikuja kunichukua wakati aliposikia taarifa kuwa natumia madawa, mana nililia sana na nilitaka hata kutoroka kambini kwasababu akili yangu ilikuwa haipo sawa kutokana na taarifa zilizozagaa kuwa mimi natumia madawa, niliumia sana na sijui nani nimemkosea ata ananifanyia hivi ila mimi nimeshamsamehe ndo changamoto za maisha lakini wameitia unyonge sana familia yangu, mamaangu alilia sana pamoja na dada zangu kuona nazushiwa taarifa hizi”. Alisema Mwinyi huku akiwa anatoka machozi.
Aidha Mwinyi amekanusha picha zilizozagaa sasaivi katika mitandao ya kijamii picha ambazo zimewekwa mbili kwa pamoja, moja ikionesha alivyokuwa zamani na moja alivyo sasa ambapo picha hizo zime tengenezwa si za ukweli na yeye Mwili wake upo vile vile.
“Jamani mimi sipo hivyo kama picha zilivyozagaa katika mitandao ya kijamii, Kisandu ule picha ukiangalia tu unaona kama si ya ukweli, kwanza uwanja gani ule tulocheza mazoezi sisi Yanga, na ukiangalia kwa nyuma kuna goli la Hand ball, sasa sisi Yanga lini tumefanya mazoezi uwanja kama huo na pia Yanga wafanye mazoezi kusiwe hata mashabiki kuangalia!, duh watu wananichafua sana ila mimi nipo vizuri na wapenzi wa Yanga na Tanzania wategemee makubwa kuliko mwanzo Kisandu”.
Jumamosi ya April 30, 2016 moja ya Gazeti la michezo nchini Tanzania ambalo ni BINGWA liliandika taarifa ndefu kuhusu mlinzi wa Yanga ambapo kichwa cha habari kilikuwa kimeandikwa “ SIRI NZITO YAFICHUKA YANGA”, NYOTA ALIYEMKUNA MAHREZ WA LEICESTER NI TEJA WA KUTUPWA, APIGWA CHINI” .
Zaidi ushahidi huo apo kwenye picha unaonesha kuwa si kweli Mwinyi hatumii madawa ya kulevya bali ni wachache wasiompenda wanamchafua.
Chanzo-Naipenda Yanga
0 comments:
Post a Comment