Thursday, August 4, 2016

Baada ya kuwasili jana usiku majira ya saa 4:30 Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Laudit Mavugo asubuhi ya leo anatarajiwa kufanya mazungumzo na viongozi wa Simba SC.

Mavugo ambaye alipokelewa na Makamu wa Rais wa Simba, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ na kupelekwa  hotelini kupumzika baada ya kukamilisha usajili wake ambao kwa asilimia zote utafanyika, ataelekea Morogoro kuungana na wachezaji wenzake waliopiga kambi Chuo cha Biblia mjini Morogoro. 
Simba wamefanikiwa kumleta straika huyo wa Vital'O ya Burundi baada ya danadana za muda mrefu na tayari zimesalia siku mbili tu kufungwa kwa dirisha la usajili wa majira ya kiangazi.
Shirikisho la Soka Tanzania bara (TFF) siku mbili zilizopita lilitangaza kuwa Agosti 6 mwaka huu ndio siku ya mwisho ya Usajili na halitathubutu kuongeza muda, hivyo timu zote zinatakiwa kujipanga kwa hilo.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video