Kujifunga
goli au kupata kadi nyekundu kwenye mechi ya kwanza unapojiunga na timu mpya kunaaminika
kuwa mwanzo mbaya zaidi wa maisha mpya soka, lakini Jeremy Menez ameanza vibaya
kwa kiwango kinachosikitisha wakati
akicheza kwa mara ya kwanza katika kikosi cha Bordeaux.
Siku mbili tu
baada ya kujiunga na timu hiyo ya Ufaransa inayocheza Ligi kuu ya nchi hiyo
maarufu kama Ligi One, akitokea AC Milan, Menez amepoteza sehemu ya nyama ya
sikio lake la kulia baada ya kukanyagwa kwa bahati mbaya na mlinzi wa Lorient,
Didier Ndong.
Tukio hilo
lilitokea baada ya kiungo huyo wa Lorient kusimamia mguu wake katika kichwa cha
mchezaji huyo mwenye miaka 29 na kusababisha majeraha hayo mabaya.
Lorient
walioumizwa na tukio, wametoa taarifa kuthibitsha kuwa mshambuliaji huyo wa
zamani wa Paris Saint-Germain anahitaji kufanyiwa upasujaji katika jereha lake kwa lengo la kuwekewa sikio lingine,
huku mchezaji wake Ndong akimuomba radhi Menez na klabu yake ya Bordeaux
kutokana na ajali hiyo ya uwanjani.
Menez alicheza
dakika 15 tu kwenye mechi hiyo ya kirafiki ambayo timu yake ilishinda mabao
matatu kwa bila.
Menez
Jumatatu ya Juma hili alisaini mkataba wa miaka miwili na Bordeaux baada ya
kudumu kwa misimu miwili ligi kuu ya Italia, Seria A.
0 comments:
Post a Comment