Wednesday, August 10, 2016

Paul Pogba ni jina ambalo limegonga vichwa vya habari kwa muda mrefu sana, lakini jana likashika zaidi baada ya kusajiliwa rasmi na klabu ya Manchester United. Safari ya soka ya Paul Pogba imeanzia mbali sana.

Pogba ni mtoto wa mwisho wa Yeo Pogba, mama jasiri alifanikiwa kuzaa watoto watatu ambao ni mapacha Florentin Pogba na Mathias Pogba pamoja na Paul Pogba mwenyewe.

Angalia hiyo picha hapo juu, ambapo mama yao Poga, Yeo Pogba akionekana amezungukwa na wanawe, katika moja ya nyumba zilizopo kwenye vitongoji vya jiji la Paris ambapo hapo ndipo aliwapowalea kuanzia udogoni mpaka wakakua kabisa.

Sasa Yeo amekuwa ni mama mwingine kabisa, mama wa mchezaji ghali kuliko wote duniani. Kabla ya usajili wake uliovunja rekodi wa paundi mil 100 kutoka Juventus kwenda Manchester United haujatangazwa, Pogba aliposti video-picha na kuandika maneno ya shukrani kwa mama yake ambaye anaamini ndiye mchango mkubwa sana kwenye maisha yake mpaka sasa.

Aliandika hivi: ‘Happy Mother’s Day kwa mama yangu, ambaye ana baraka nyingi za Mungu.'

'Nimekuwa ni mwenye bahati kubwa kuwa mwanao, ninajivunia sana wewe kuwa mama yangu, mtoto wa mama!'
Mara ya kwanza walikuwa wakiishi kwenye nyumba iliyopo eneo la Renardiere housing estate huko Roissy-en-Brie kabla ya kuhamia kunako jijini Paris ambapo, Pogba na kaka zake mapacha Mathias na Florentin walipata makuzi yao huko. 

Mama yao alijitahidi sana kueneza upendo kwa watoto wake, hali iliyosababisha kupendana nyakati zote.

'Yeo alipenda watoto wake wote kuwa na tabia njema kuanzia siku ya kwanza nilipomuona, bila ya kujali hali ya kiuchumi waliyokuwa nayo,' alisema moja ya majirani waliokuwa wakiishi na mama yao Pogba.

'Alikuwa akiwafunza tabia njema na kuheshimu kila mtu wanayemwona mbele yao,' chanzo kiliongeza. 'licha ya kuishi maisha magumu, lakini aliamini siku moja watoto wake wote wangefika sehemu fulani ya mafanikio.

'Kama mtu alifanya jambo la makusudi kuwaudhi au kuwafanyia jambo lolote baya, Yeo hakujali hata kidogo isipokuwa kuendelea kuwapa watoto wake furaha.'

Ferguson atamkumbuka vizuri mama huyu, pale Pogba alipokuwa akipata wakati mgumu klabuni hapo kabla ya kuondoka kwenda Juventus.

Yeo na familia yake nzima, walimfuata Ferguson na kumlazimisha ampe mwanawe ruhusa ya kuondoka na kwenda mahali pengine. Hiyo ilikuwa ni mwaka 2012. Alisema hivi: 'Mimi na kaka zake Paul kwa pamoja tumeamua kwamba, Pogba hatasaini mkataba mpya.' Baada ya kitendo hicho Ferguson alikasirika na kutomchezesha tena Paul.

Yeo anaendelea kusema: 'Ilifikia hatua hadi Pogba akalia ofisini kwa Ferguson kutokana na namna alivyokuwa akifanyiwa.'

Sasa Yeo ndio ameibuka shujaa baada ya mitihani yote aliyompambania mwanawe.

Wakati Pogba akiwa kwenye ndege kuelekea jijini Manchester kwaajili ya kusaini mkata na timu hiyo, Yeo alikuwa karibu kabisa na mwanawe akiwa mwenye uso wa bashasha kabisa.

Malkia huyo wa nguvu wa Pogba kama mwenyewe anavyopenda kumwita 'Super Mum', aliachana na mume Antoine wake mwaka 1996, wakati Pogba akiwa na umri wa miaka miwili tu.


Licha ya kuachana na mkewe, lakini aliendelea kuishi karibu kabisa na iliko familia yake.

Antoine, ambaye ni baba mzazi wa Pogba na kaka zake alikuwa muajiriwa wa moja ya makampuni ya mawasiliano huko N'Zerekore nchini Guinnea akiwa kama mhandisi ambapo aliacha kazi miaka ya 1990.

 Baadaye akawa mwalimu ambapo mara nyingi aliwachukua watoto wake kwenda kucheza mpira na mara nyingine kuangalia mpira hasa kwenye timu za Paris St Germain, na Marseille. 

Enzi hizo anawachukua kwenda kucheki soka, watoto wake wote walikuwa washabiki wakubwa wa Marseille na taratibu wakaanza kufanikiwa kwenye soka na ndipo Mathias na Florentin walipopata nafasi ya kuchezea taifa lao la Guinnea.

Paul alikuwa bora zaidi ya wenzake, na ni mama yake (Yeo) ndiye alimshawishi kuchezea Ufaransa,' alisema moja ya majirani hao.

Itaendelea kesho.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video