Wakati huu Manchester United wanajiandaa kuanza msimu mpya wa Ligi kuu Soka ya England, bosi wake, Jose Mourinho yuko 'bize' sana katika Ofisi yake iliyopo Carrington.
Page ya Instagram ya Mourinho ime-share picha ikimuonesha Mreno huyo akiwa amekaa mezani kwake akisoma vitu kwenye Tablet yake.
Kocha huyo wa zamani wa Chelsea na Real Madrid, mezani kwake alisambaza nyaraka mbalimbali na nyuma kuna TV kubwa ya kucheki mambo yanavyokwenda duniani.
Man united wamefurahia maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu ambapo mechi ya mwisho walishinda 5-2 dhidi ya Galatasaray ya Uturuki, lakini mechi dhidi ya Manchester City iliyotakiwa kuchezwa huko Beijing, China ilifutwa kutokana na hali mbaya ya hewa.
Mabadiliko aliyoleta Mourinho kwenye kikosi cha Manchester United yameelezwa kwa kifupi na kiungo wake,
Morgan Schneiderlin ambaye ameiambia Tovuti ya Manchester United wanavyojisikia wakati huu wa maandalizi ya msimu mpya wa mashindano.
"Naweza kuona tabasamu na furaha kubwa wakati wa mazoezi, kitu ambacho ni kizuri"-Schneiderlin.
0 comments:
Post a Comment