Jack Wilshere (kushoto) akizungumza na Arsene Wenger |
Arsenal wanajiandaa kumruhusu Jack Wilshere kuondoka klabuni hapo kwa mkopo ili kutafuta timu atakayopata nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza.
Wilshere amekuwa akikaa benchi tangu msimu huu wa Ligi kuu ya Soka ya England uanze kwasababu wakati wa maandalizi ya msimu mpya (Pre-season) alikuwa nje ya dimba kutokana na majeraha
Washika Bunduki hao wa London wamebakiwa na siku mbili za kutafuta mbadala wa Wilshere kwani dirisha la usajili wa majira ya kiangazi litafungwa Jumatano hii saa 6:00 usiku.
Nyota huyo wa miaka 24 pia ameachwa na Sam Allardyce katika kikosi chake cha kwanza tangu ateuliwe kuwa kocha mkuu wa Timu ya Taifa ya Kandanda ya England.
Allardyce aliweka wazi kuwa Wilshere anatakiwa kupata nafasi ya kucheza sana kandanda kama anataka kurudishwa timu ya Taifa.
0 comments:
Post a Comment