Saturday, August 13, 2016

Wapinzani wa Machampion wa ligi kuu Tanzania Bara, Yanga SC, Mo Bejaia wamefanya mazoezi yao ya mwisho jana jioni kabla ya mechi ya Kombe la Shirikisho inayotarajia kupigwa leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kocha wa MO Bejaia, Nasser Sandjak alisema mchezo huo lengo lao ni kushinda, ingawa anaiheshimu Yanga.

"Nimefarijika kukaribishwa vyema Tanzania na suala la mchezo wa kesho (leo) ni kushindana. Naiheshimu Yanga kwa kuwa nimecheza nayo kabla. Ni timu nzuri yenye ushindani wa kweli". Alisema Sandjak.

Mo Bejaia kutoka nchini Algeria  katika matizi yao walionekana wako tayari kwa mechi hiyo ambayo kama watashinda watakuwa wamefikisha angalau asilimia 90 za kutinga hatua ya nusu fainali.

Lakini Yanga pia wanataka kushinda mchezo huo kuinua matumaini yao ya kufikia hadi asilimia 60 za kuweza kusonga mbele.

Katika mechi ya kwanza ambazo zilikutana nchini Algeria, Bejaia walishinda kwa bao 1-0.

Licha ya kwamba Young Africans kuwa na pointi moja, bado ina nafasi ya kushika nafasi za juu katika kundi la A ambalo msimamo wake unaongozwa na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), huku Mo Bajaia ya Algeria na Medeama ya Ghana, zina pointi tano kila moja. Wakati Young Africans wanacheza na Mo Bajaia iliyoshinda mchezo wa kwanza huko Algeria, Medeama itakipiga na TP Mazembe. 
Mchezo huu utachezeshwa na waamuzi kutoka Ethiopia ambako katikati atakuwa Bamlak Tessema Weyesa akisaidiwa na Kindie Mussie mstari upande wa kusini na Temesgin Samuel Atango katika mstari wa Kaskazini upande wa wakati Mwamuzi wa Akiba atakuwa Haileyesus Bezezew Belete. 
Kamishna wa mchezo atakuwa Gaspard Kayijuka kutoka Rwanda wakati Desire Gahuka wa Burundi atasimamia ufanisi wa waamuzi wa mchezo na Mratibu Mkuu wa mchezo atakuwa Isam Shaaban kutoka Sudan. Mratibu huyo anatarajiwa kuwasili leo Agosti 10, 2016 wakati waamuzi watatua kesho Agosti 11, 2016 na msimamizi wa waamuzi atatua Ijumaa Agosti 12, 2016.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video