Hamad Juma |
Beki wa kati wa Wekundu wa Msimbazi Simba SC, Novaty Lufunga aliyepata majeraha mwishoni mwa Juma lililopita anaendelea vizuri kiafya.
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Hajji Sunday Manara amethibitisha kuwa Lufunga huenda akaanza mazoezi leo.
"Nimeulizwa na watu wengi kuhusu hali ya mchezaji wetu Novart Lufunga aliyeumia juzi, Niwataarifu anaendelea vyema na In Sha Allah leo ataanza mazoezi". Amesema Manara.
Manara pia amefafanua kuwa Mlinzi wa kulia wa Simba aliyeanguka bafuni wiki iliyopita, Hamad Juma anaendelea kuimarika zaidi kiafya.
"Mchezaji Hamadi Juma aliyeanguka bafuni wiki iliyopita kwa sasa yupo kwao Tanga na ndani ya siku chache zijazo ataanza mazoezi na timu baada ya hali yake kuzidi kutengamaa". Ameeleza Manara.
Simba inajiandaa na mechi ya tatu ya Ligi kuu Soka Tanzania Bara itakayochezwa Septemba 7 mwaka huu Uwanja wa Uhuru, Dar es salaam, dhidi ya Ruvu Shooting ya Pwani.
Mpaka sasa Simba inashika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kuu ikijikusanyia pointi 4 kwenye mechi mbili ilizoshuka dimbani, sawa na Azam FC wenye pointi 4 kileleni, lakini wanafaida nzuri ya mabao ya kufunga na kufungwa.
0 comments:
Post a Comment