Baada ya mkutano mkuu wa wanachama wa Yanga SC kufanyika kesho Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam, jioni kikosi cha Wanajangwani kitacheza mechi ya kirafiki uwanja wa Taifa dhidi ya Mtibwa Sugar.
Kocha mkuu wa Yanga anaamini mchezo huo utakuwa msaada mkubwa kwa benchi lake la ufundi kujua kasoro zilizopo kabla ya Agosti 13 kucheza na MO Bejaia katika mechi ya marudiano ya kombe la Shirikisho barani Afrika.
"Katika mechi za ushindani timu huitaji ushindi, Mashabiki wetu huihitaji kuona tukishinda. . Lakini hatuna matokeo mazuri katika michuano ya kombe la shirikisho kwa kuwa kuna makosa ambayo tunafanya na yametugharimu. . Kama unavyoona hapa tunaendelea kujifua ili kuzuia makosa hayo yasijirudie kwa michezo ijayo. . " Pluijm akikaririwa na ukurasa maarufu wa facebook wa Naipenda YANGA .
Kuhusu mechi ya kirafiki, Pluijm alisema:"Mchezo wa kirafiki dhidi ya Mtibwa sugar tunategemea utakuwa muhimu kwetu kama kipimo kujua wapi tunakasoro kabla ya kuwakabili Mo Bejaia" .
0 comments:
Post a Comment