Klabu ya Simba , Jumapili uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam, inatarajia kucheza mechi ya pili ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya URA ya Uganda.
Benchi la ufundi likiongozwa na kocha Mcameroon, Joseph Omog, akisaidiwa na Mganda, Jackson Mayanja, limefurahi kupata mchezo huo mwingine wa kujipima ubavu.
"Nashukuru sana uongozi, wamejaribu kutupatia benchi la ufundi mechi ya pili na ya kimataifa, itatusaidia sana kuona level ya timu yetu, kwasababu tumeona ikicheza mechi ya kimataifa moja na sasa tunacheza na URA". Amesema Mayanja na kuongeza: "URA ni timu nzuri kutoka Uganda na itawasaidia wachezaji wenyewe kupata level ya fitness na level ambayo tunachezea, wachezaji wengi hawajacheza mechi ile (dhidi ya AFC Leopard), nao watapata nafasi, nasisi benchi la ufundi tutapata muda wa kuwaona".
Nyota wapya waliocheka na nyavu kwenye mechi dhidi ya AFC Leopard ambayo Simba walishinda 4-0, Shiza Kichuya na Laudit Mavugo (goli moja kila mmoja) wanatazamiwa kuanza katika mechi hiyo ambayo itawapa fursa nyingine mashabiki kukiona kikosi chao.
0 comments:
Post a Comment