PREMIER LEAGUE: Vilabu vya Ligi Kuu England sasa vimetumia zaidi ya paundi bilioni moja kwenye dirisha hili la usajili. Kiasi hiko cha fedha kimevunja rekodi ya msimu uliopita. Rekodi hiyo imevunjwa wiki iliyopita wakati Manchester City walipomsajili kipa kutoka Barcelona Claudio Bravo na kufikisha jumla ya paundi mil 880. Msimu uliopita jumla ya paundi mil 850 zilitumika katika usajili.
PSG: Paris Saint-Germain wanafikiria kumuuza David Luiz baada ya Chelsea kuweka mezani kiasi cha paundi mil 32 ili kumrejesha beki wao wa zamani Darajani.
FRANCE: Kiungo mshambuliaji wa Newcastle United Moussa Sissoko ameruhusiwa kuondoka katika kambi ya timu ya taifa ya Ufaransa ili kukamilisha uhamisho wa kujiunga na klabu ya Tottenham Hotspur.
LEICESTER: Mabingwa Watetezi wa Premier League Leicester City wamefikia muafaka wa kumsajili nyota wa kimataifa wa Algeria Islam Slimani kutoka klabu ya Sporting kwa ada ya euro mil 35 (ESPN FC).
ARSENAL: Crystal Palace wana matumaini makubwa wa kumsajili kiungo wa Arsenal Jack Wilshere kwa mkopo wa msimu mzima kabla ya dirisha la usajili kufungwa rasmi leo usiku.
- Vilevile Arsenal wamemtoa kwa mkopo wa msimu mzima beki wao Calum Chambers kwenda Middlesbrough.
- Werder Bremen wameripotiwa kufikia makubaliano na Arsenal kumchukua winga Serge Gnabry na katika dili hilo Bayern Munich watahusishwa pia.
LIVERPOOL: Christian Benteke ana shauku kubwa ya kuthibitisha ubora wake kwenye klabu yake mpya ya Crystal Palace na haamini kwamba alishindwa kuonesha makali yake kunako klabu ya Liverpool.
MAN UNITED: Kiungo wa Manchester United Mjerumani Bastian Schweinsteiger amesisitiza kwamba ndoto yake ilikuwa ni bado kubaki Old Trafford lakini amesema kwamba safari yake baada ya kutoka United ni kuelekea nchini Marekani kucheza Major League Soccer.
- United bado wana nia ya kumbakisha beki wao Marcos Rojo licha ya tetesi za kutakiwa na klabu ya Valencia ya nchini Uhispania.
0 comments:
Post a Comment