Jumatano hakutakuwa na mchezo wowote wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara kutokana na wachezaji wa Yanga SC kwenda katika timu za Taifa.
Mabingwa watetezi wa VPL wachezaji wake 9 watakuwa katika majukumu na timu zao za Taifa hivyo wamelazimika kuvunja kambi jana na wataingia kambini Jumatatu Ijayo ili kujiandaaa na mechi yao na Ndanda ya Mtwara itakayochezwa Mtwara siku ya Jumatano Septemba 7,hivyo mchezo dhidi ya JKT Ruvu uliotakiwa kupigwa Agosti 31 unaendelea kuwa kiporo.
Katika orodha hiyo ya wachezaji 9, wanandinga 6 wa Yanga wanajiunga na Timu ya Taifa ya kandanda ya Tanzania, Taifa Stars, ambao ni Deogratius Munishi ,Kelvin Yondani ,Vicent Andrew ,Mwinyi Haji ,Juma Mahadhi na Simon Msuva
Kwa upande wa kimataifa, Tayari Vicent Bossou imeripotiwa kusafiri jana usiku kuelekea kwao Togo kujiunga na kambi ya timu ya Taifa ya nchi hiyo.
Wengine ni Haruna Niyonzima anayekwenda kujiunga na Timu ya Taifa ya soka ya Rwanda, Amavubi, huku Amissi Tambwe akielekea kujiunga na timu ya Taifa ya Burundi, Intamba Murugamba.
0 comments:
Post a Comment