Wednesday, August 17, 2016

Thierry Henry amefichua kitu gani hasa mchezaji anapaswa kuwa nacho ili kucheza chini ya Gurdiola na kueleza sababu za Guardiola kutodumu kwenye timu moja kwa muda mrefu.
Henry alishawahi kucheza chini ya Guardiola akiwa Barcelona na amesema kwamba, si kitu rahisi hata kidogo kufundishwa na Guardiola
Alipotakiwa kutoa ufafanuzi juu ya kauli yake, Henry alisema "Mazoezi yake ni magumu sana. Anapenda kila mchezaji kujituma ili kutawala mchezo. Anataka kudhibiti kila kitu uwanjani. Anataka kujua kila kitu. Anataka kuwa bosi wa kila kitu.
"Ni vigumu sana. Unapaswa kuwa tayari kuendana naye.
"Si kitu rahisi kufanya. Mwenyewe ameshawahi kusema: baada ya miaka miwili au mitatu basi anaondoka, hataki kukaa kwa muda mrefu kutokana na kazi kubwa anayofanya, Si mtu rahisi kupambana naye. Lakini amekuwa na mafanikio kila sehemu alipofanya kazi."

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video