Saad Kawemba |
Wakati huu picha ikisambaa ikimuonesha mshambuliaji wa Azam FC, Raia wa Ivory Coast, Kipre Tchetche akitambulishwa katika klabu ya Al Nahdha ya Oman, uongozi wa Wanalambalamba umesema picha hiyo ina zaidi ya mwezi mmoja kwenye mtandao na wao wameiona.
Afisa Mtendaji mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba ameiambia MPENJA SPORTS asubuhi kwamba wao hawafahamu chochote, wanachojua Kipre bado wana mkataba naye.
Picha ya Tchetche inayoendelea kusambaa ikidaiwa akitambuliswa Al Nahdha ya Oman |
Kawemba ameeleza kwamba kama kuna klabu inamtaka Kipre au imemsainisha mkataba, lazima itatua Azam FC kuwasilisha nyaraka.
"Tulishasema ana mkataba na klabu (Kipre), Transfer yoyote inapofanyika, klabu lazima ituulize. Akisaini mkataba lazima karatasi zifike Azam, lazima watazungumza nini wanachotaka na nini sisi tunataka". Amesema Kawemba.
Hata hivyo, Tchetche bado hajawasili Chamazi mpaka sasa wakati wenzake akiwemo pacha wake, Michael Balou, walishaanza mazoezi.
Kuhusu hilo, Kawemba amefafanua kuwa mchezaji huyo anaufahamu utaratibu wa klabu pindi unapochelewa kujiunga na timu.
Kauli ya Kawemba inaaminika kwamba Tchetche hana ujanja na kama atarudi basi atachukuliwa hatua za kinidhamu.
Kipre amebakiza mkataba wa mwaka mmoja na Azam FC.
0 comments:
Post a Comment